Isaiah 41:1-6

Msaidizi Wa Israeli


1 a“Nyamazeni kimya mbele zangu, enyi visiwa!
Mataifa na wafanye upya nguvu zao!
Wao na wajitokeze, kisha waseme,
tukutane pamoja mahali pa hukumu.


2 b“Ni nani aliyemchochea mmoja kutoka mashariki,
akimwita katika haki kwa utumishi wake?
Huyatia mataifa mikononi mwake,
na kuwatiisha wafalme mbele zake.
Huwafanya kuwa mavumbi kwa upanga wake,
huwafanya makapi yapeperushwayo na upepo kwa upinde wake.

3 cHuwafuatia na kuendelea salama,
katika njia ambayo miguu yake haijawahi kupita.

4 dNi nani aliyefanya jambo hili na kulitimiliza,
akiita vizazi tangu mwanzo?
Mimi, Bwana, ni wa kwanza
nami nitakuwa pamoja na wa mwisho:
mimi Bwana ndiye.”


5 eVisiwa vimeliona na kuogopa,
miisho ya dunia inatetemeka.
Wanakaribia na kuja mbele,

6 fkila mmoja humsaidia mwingine
na kusema kwa ndugu yake, “Uwe hodari!”
Copyright information for SwhKC